November 27, 2020

 


KIUNGO mchezeshaji wa Simba, Clatous Chama, ameibuka na kuweka wazi shauku yake ya kumuona kaka yake, Adrian Chama akijiunga naye ndani ya kikosi hicho cha Simba.

 

Chama ameongeza kuwa, anatamani ndugu yake huyo atue Simba kutokana na kuwa na uwezo mkubwa kumzidi hata yeye. Adrian anayecheza nafasi ya beki wa kati ndani ya kikosi cha Zesco United, alijiunga na kikosi hicho Julai Mosi, 2019.

 

Mzambia huyo mwenye mabao manne katika Ligi Kuu Bara, aliweka wazi suala hilo la kutamani Adrian anayeichezea Zesco United ya Zambia wakati akijibu swali aliloulizwa kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram.

 

Chama aliulizwa kuwa kama anatamani Adrian mwenye miaka 31 asajiliwe Simba na kusema ndiyo huku akiongeza kwamba Adrian ana uwezo mkubwa wa kisoka kumzidi yeye. “Ndiyo ndiyo, kwa sababu Adrian ana uwezo kuzidi mimi.”

 

Chama amekuwa akitajwa kuwa mchezaji bora zaidi wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa misimu miwili akiwa ametwaa tuzo hiyo mara mbili.

2 COMMENTS:

  1. Anatamani ndugu yake aje simba. Unaandika uwongo simba hawajasema chochote wala hawajui chochote

    ReplyDelete
    Replies
    1. Maneno ya Chama sio ya Simba au kiswahili chenga mzee!!!

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic