November 27, 2020


NYOTA wengi duniani wameendelea kutoa pole kutokana na kifo cha Diego Maradona amefariki akiwa na umri wa miaka 60, siku za mwisho alifanyiwa upasuaji wa ubongo akiwa anaedelea vizuri na kuruhusiwa kutoka hospitali.


Miongoni mwa mastaa ambao wametoa kauli kuhusu kifo cha Maradona ni pamoja na Lionel Messi raia wa Argentina ambaye alikuwa anatajwa kuwa mrithi wa Maradona na aliwahi kufundishwa na mkongwe huyo.


Messi amesema kuwa ni siku ya kusikiitika kwa familia ya wanasoka wote duniani na Argentina inasikitika licha ya kuondoka bado anaishi.


Kifo kimemkuta akiwa nyumbani, mara baada ya kupata kifungua kinywa juzi, Novemba 25 Maradona inaelezwa kuwa alimuita mpya wake, Johny Esposito na kutamka maneno mafupi,' Me siento mal' akimaanisha kuwa hajisikii vizuri kisha akarejea kitandani kulala.


Muuguzi wa kike ambaye alikuwa akisaidia kumuuguza baada ya kutoka hospitali baada ya kuona hivyo akapiga simu kuomba gari ya wagonjwa, 'ambulance' lakini hadi gari linafika nyumba aliyokuwa amepangisha alipokuwa akikaa baada ya kutoka hospitali Novemba 11 alikuwa amekata kauli.


Staa huyo wa zamani wa Napoli na Barcelona inaelezwa kuwa alipata shambulio la moyo na alikata kauli majira ya saa sita mchana kwa muda wa Argentina na taarifa zinaeleza kuwa taratibu za kuuaga mwili wa Maradona zitafanyika katika Ikulu ya Argentina.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic