November 27, 2020


 BAADA ya Arstica Cioaba kufutwa kazi ndani ya Klabu ya Azam FC, jana Novemba 27 mrithi wa mikoba yake ni Vivier Bahati ambaye alikuwa Kocha Msaidizi.

Cioaba amesitishiwa mkataba wake pamoja na kocha wa viungo, Costel Birsan ambaye alikuwa akifanya naye kazi kwa ukaribu.

Mrithi wa mikoba yake kwa muda amepewa mechi mbili ambapo ya kwanza ni ile dhidi ya Biashara United pale Uwanja wa Karume na ya pili ni ile dhidi ya Gwambina FC ya Mwanza Uwanja wa Gwambina Complex. 


Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa mchakato wa kufutwa kazi kwa makocha hao ni makubaliano ya pande zote mbili baada ya kukaa kutokana na mwendo mzima wa Azam FC.


Ikiwa imecheza jumla ya mechi 12 ndani ya msimu wa 2020/21 ilishinda mechi nane na kulazimisha sare moja mbele ya JKT Tanzania kwa kufungana bao 1-1 Uwanja wa Azam Complex imepoteza mechi tatu ambapo ya kwanza ilikuwa dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri.


Mechi ya pili ilikuwa dhidi ya KMC Uwanja wa Uhuru na ya tatu ilikuwa dhidi ya Yanga Uwanja wa Azam Complex na zote ilipoteza kwa kufungwa bao mojamoja.


Akiwa ndani ya Azam FC, Cioaba jumla alikiongoza kikosi hicho kwenye mechi 50 ambapo alishinda 28, sare 11 na kupoteza 11 kwa msimu wa 2019-20.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic