November 10, 2020


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa malengo makubwa kwa msimu wa 2020/21 ni kuendelea kupata pointi tatu kwenye mechi zote watakazocheza ili kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.


Baada ya kumaliza Dar Dabi ya kwanza Novemba 7 kwa kutoshana nguvu ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Simba Uwanja wa Mkapa, hesabu yao inayofuata ni dhidi ya Namungo FC.


Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Novemba 22, Uwanja wa Uhuru na unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili zinazonolewa na makocha wageni.


Yanga ipo chini ya Cedric Kaze raia wa Burundi anakutana na Hitimana Thiery raia wa Rwanda ambaye yupo ndani ya Namungo.


Akizungumza na Saleh Jembe, Kaze amesema kuwa watapambana kufanya vizuri ili kuwa bora kwenye mechi zao zijazo.


"Bado tuna kazi ya kufanya kwa ajili ya mechi zetu zijazo, ninaamini kwamba tutarudi uwanjani tukiwa bora na imara zaidi," amesema.


Kwa sasa Ligi Kuu Bara na Ligi Daraja la Kwanza zimesisimama kupisha maandalizi ya mechi za timu za Taifa ambapo Taifa Stars itashuka uwanjani Novemba 13 kumenyana na Tunisia kuwania kufuzu Afcon, nchini Cameroon, 2021. 

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic