DEUS Kaseke kiraka wa Yanga amesema kuwa ubora wake ndani ya uwanja unatokana na kufuata maelekezo ambayo anaelekezwa na mwalimu wake ayafanye.
Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze haijafungwa na timu zote zilizo ndani ya tatu bora ikiwa ni pamoja na Simba iliyo nafasi ya tatu na pointi 23 pamoja na Azam iliyo nafasi ya pili na pointi 23.
Novemba 25, Uwanja wa Azam Complex Kaseke alifunga bao la ushindi kwa timu yake wakati ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam Complex.
Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote mbili kuwa kwenye ubora, Kaseke alifunga bao hilo dakika ya 48 kwa pasi ya Yacouba Sogne.
Kaseke amesema:"Kufuata maelekezo ambayo ninapewa na mwalimu ninafanya nikiwa ndani ya uwanja jambo ambalo linanifanya ninakuwa bora.
"Suala la namba yangu mimi kucheza uwanjani popote pale ninacheza hivyo sina mashaka nitazidi kupambana kwa ajili ya kutimiza majukumu yangu," .
Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa imecheza mechi 12 bila kupoteza ndani ya dakika 1,080 imefunga mabao 14 na kufungwa mabao manne.
Ina kibarua cha kumenyana na JKT Tanzania, Novemba 28 Uwanja wa Mkapa saa 10:00 jioni.
0 COMMENTS:
Post a Comment