November 10, 2020


 IMEELEZWA kuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachovaana na timu ya Taifa ya Tunisia Novemba 13.


Mbwana Samatta ambaye ni mshambuliaji jina lake lipo kwenye orodha ya wachezaji 27 walioitwa kuunda kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.


Kwa sasa Stars chini ya Kocha Mkuu, Ettiene Ndayiragije imeweka kambi nchini Uturuki ambapo nyota huyo anacheza nchini humo.


Habari zinaeleza kuwa Samatta hayupo kwenye mazoezi na timu ya Taifa ya Tanzania kwa kuwa ana matatizo ya kiafya na ameshauriwa na madaktari kutocheza ili arejee kwenye ubora wake.





5 COMMENTS:

  1. Bainisha matatizo ya kiafya yapi?too general.

    ReplyDelete
  2. Imeelezwa na nani?habari ambazo hazina source msituchoshe nazo hata mwandishi wa hii habari hajulikani.

    ReplyDelete
  3. Hizi habar za kuunga unga ambazo hazina Source sio za kuziamini sana.

    ReplyDelete
  4. Hii blog kwakwel huaga haina source of information ndo tatizo lao kwahiyo hizi habari mzipuuze kabisaaa

    ReplyDelete
  5. Acha kuisoma kwani nani anakulazimisha???

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic