RAIS wa Jamhuri ya Tanzania, John Pombe Magufuli amesema kuwa anawatakia kheri wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo ina mchezo dhidi ya Tunisia kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya Afcon.
Magufuli amesema kuwa Watanzania wanahitaji ushindi kwa kuwa wamechoka kushindwashindwa.
"Ninapenda kuitakia kheri timu yetu ya Taifa ya Taifa Stars kwenye mechi yake dhidi ya Tunisia pamoja na bondia Hassan Mwakinyo ambaye naye ana pambano leo.
"Watanzania tunataka ushindi tumechoka kushindwa shindwa.
"Tutaanza pia kuanza kutenga fedha kidogokidogo kwa ajili timu za Taifa kwa ajili ya kujiandaa," amesema Magufuli.
Stars ambayo ipo kundi J leo Novemba 13 itacheza mchezo wake wa tatu dhidi ya Tunisia na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa Novemba 17, Uwanja wa Mkapa.
HAMNA KITU HAPO
ReplyDeleteBure kbsa ovyoo
ReplyDelete