November 26, 2020


 CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga  amesema kwamba atazidi kuwapa nafasi wachezaji wa timu B kwa sababu anataka wajione ni sehemu ya kikosi cha timu hiyo na anaamini watafanya vizuri kutokana na uwezo walionao.

 

 Omary Chibada nyota wa Yanga kutoka kikosi B amekuwa wa kwanza kupandishwa baada ya kufanya vizuri kwenye mechi za kirafiki jambo lililomfungulia njia ya kuingia kikosi cha kwanza.

 

 Kaze amesema:”Wapo wachezaji wengi ambao wanacheza timu B na wana uwezo mkubwa ndani ya uwanja, taratibu nitawapa nafasi huku pia ili waendelee kukomaa na kuonyesha kile ambacho wanacho.

 

“Najua kwamba kila mchezaji ana shauku ya kuanza kikosi cha kwanza lakini haiwezi kuwa rahisi ni lazima kila mmoja apambane kwenye mazoezi pamoja na mechi ambazo tunacheza kwani ushindani ni mkubwa,” .

 

Raia huyo wa Burundi jana alikiongoza kikosi chake kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.


Bao la ushindi kwa Yanga lilifungwa na Deus Kaseke ambaye anakuwa mzawa wa pili kufunga bao ndani ya Yanga, bao la kwanza lilifungwa na Wazir Junior wakato Yanga ikishinda kwa mabao 2-1 dhidi ya KMC.

 

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic