KIBARUA cha Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, huenda kikaota nyasi kutokana na mfululizo wa matokeo yasioridhisha.
Hatua hiyo inakuja ikiwa baada ya kutoka kupokea kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Istanbul Basaksehir kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Gazeti la The Mail limeripoti kuwa mabosi wa United wameanza mazungumzo na aliyekuwa kocha wa Totenham Hotspurs, Mauricio Pochettino, ili aokoe jahazi la timu hiyo ambalo linaonekana kuzama wakati Solskjaer ameishiwa mbinu za kuinusuru.
Pochettino ambaye yupo jijini London kwa wiki mbili sasa, hivi karibuni amenukuliwa akisema yupo mbioni kurudi kufundisha bila kutaja ni klabu gani atakayojiunga nayo.
United wana kazi ngumu ambapo Novemba 8 mwaka huu watakawavaa Everton kwenye mchezo wa Ligi Kuu England (EPL) na kama wakifungwa watajikuta wapo nafasi 17 kwenye msimamo wa ligi na hii kuonyesha kila dalili za Ole kufukuzwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment