November 6, 2020

 


KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga, Carlos Carlinhos anatarajia kuukosa mchezo wa dabi ya Simba na Yanga utakaochezwa kesho huku kiungo Haruna Niyonzima, akirejea kwa nguvu kuwavaa watani wao hao.

 

Carlinhos aliumia kisigino katika mazoezi yaliyofanyika hivi karibuni kwenye kambi ya timu hiyo AVIC Town iliyopo Kigamboni jijini Dar kulikosababisha akose michezo minne dhidi ya Polisi Tanzania, KMC, Biashara United na Gwambina.

 

Aidha Niyonzima ambaye alikuwa akisumbuliwa na Malaria, amesharejea tayari kwa kujiandaa na mechi ya watani kesho Uwanja wa Mkapa.


 Daktari wa Yanga, Shecky Mngazija amesema kuwa, hali ya kikosi hicho ipo vizuri majeruhi wote wamekaa sawa akiwemo Niyonzima.


“Carlinhos hatoweza kucheza mechi ya watani wa jadi dhidi ya Simba kwa kuwa hayupo na kikosi kwa muda mrefu hajafanya mazoezi, lakini kiafya anaendelea vizuri, hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachoivaa Simba na kuwa hajafanya mazoezi.

 

“Niyonzima yeye amerejea kikosini ameshaanza mazoezi yupo fiti, hivyo suala la kupangwa ama kutopangwa katika mchezo huo ni jukumu la kocha,” amesema Mngazija.


Chanzo Championi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic