November 13, 2020



KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya England, Gareth Southgate amesema kuwa alitumia muda mrefu kuzungumza na Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp kuhusu suala la mchezaji wake Joe Gomez kuumia.


Gomez  beki wa Klabu ya Liverpool kwa sasa anatibu jeraha la goti ambalo alipata kwenye mazoezi na timu yake ya Taifa ya England jambo linalofaya aongeze idadi ya mabeki majeruhi  ikiwa ni pamoja na Virgil van Dijk, Fabinho na Trent Alexander-Arnold ambao nao pia wapo nje kwa sasa kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.


Southgate amesema kuwa  Gomez,  ambaye alicheza mechi sita kwenye siku 19 nyuma maumivu yake siyo kwa timu ya Taifa ya England bali pia ni kwa timu yake ya Liverpool ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England chini ya Kocha Mkuu, Klopp.

Kocha huyo amesema amekuwa na maongezi ya muda mrefu na Jurgen Klopp ili kumuondoa wasiwasi juu ya wachezaji wake kwa kuwa anahofia kukosa wachezaji wengi ambao ni muhimu kwenye kikosi chake.

" Nimekuwa na mawasiliano ya muda mrefu na Jurgen. Wote tuna mashaka juu ya kumkosa mchezaji muhimu lakini hakuna cha kufanya kwa sasa hasa ukizingatia kwamba majeraha yake hakuna ambaye alikuwa anatarajia inaweza kutokea.


"Tunahitaji kuangalia kalenda na kujua mambo yatakuaje lakini kwa bahati mbaya sana ratiba imebana na kwa namna yoyote ile nina amini kutakuwa na njia ya kutoka katika haya," amesema.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic