UONGOZI wa Simba umesema kuwa umepnaga kufanya usajili mkubwa ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya kuboresha kikosi hicho ambacho kinashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba ina kibarua cha kucheza na Plateu United ya Nigeria mchezo wa kwanza utachezwa ugenini na ule wa pili utachezwa Uwanja wa Mkapa.
Habari zinaeleza kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye hesabu za Simba ni pamoja na Mukoko Tonombe na Tuisila Kisinda ambao ni viungo wa Yanga.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa mpango mkubwa uliopo kwa sasa ni kufanya maboresha na watafanya jambo kubwa ambalo litawashangaza wengi.
Manara amesema:"Simba itafanya usajili mkubwa kwenye dirisha dogo Desemba 15 hivyo kama kocha atamhitaji mchezaji yoyote tutampata.
"Simba inahitaji wachezaji wazuri kila Mtanzania akae karibu kuona kwamba mchezaji mmoja anaingia ndani ya Simba, nazungumza masuala ya uhalisia katika yale ambayo tunayafanya.
Kuhusu ishu ya usajili wa Mukoko na Tonombe wa Yanga amesema:"Majina yao kama ni wao ama wapo wengine itajulikana kwani kwa sasa sio wakati wa usajili mpaka muda utakapofika hapo itajulikana.
"Tutasajili wachezaji wazuri,hesabu za kusajili wachezaji zipo kwa kuwa wengi wanapenda kucheza Simba basi nina uhakika kwamba dirisha la usajili litakapofunguliwa Desemba 15 labda dirisha lisifunguliwe," amesema.
Manara awasajili kisinda na mukoko??aache kuwafariji mikia wenzie,
ReplyDeleteAcha umbulula kwani Kuna mahali manara kasema anawasajili hao kina mukoko
DeleteToa evidence
DeleteIla me sijaona manara alippwataja hao walchezaji mbona
ReplyDeleteIla me sijaona manara alippwataja hao walchezaji mbona
ReplyDeletehata mimi cjaona manara akiwataja au kiongozi yeyote ni mwandishi ndo kawataja jaman
DeleteMwandishi anajitengenezea debate, kuchonganisha Kama huna hbr ya ukweli uache.
ReplyDeleteMzungu pori anawafanganya huyo mhindi hana hela za usajili
ReplyDeleteHatuna mpango na Tuisila sisi tunamtaka Tonombe,niliandika humu wakati watu wanazungumzia issue ya chama,nikasema labda mukoko simba,mkadhani natania.
ReplyDeleteKwa Namna nilivosikia mimi mchezaji huyo kawejewa dau la kumtajirisha mtu na kuwa kila kitu tayari
ReplyDeleteHahaha kwahyo manala ni mzungu poli jaman apana us seme hvyo manala ame sema wata fanya usajil kila mtu ashangae ila mwandsh aka wasema kua wana tajwa mandsh wajanja xana wachongansh
ReplyDelete