KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa hesabu kubwa kwa sasa ndani ya kikosi hicho ni kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Plateau United ambayo ni imara kwenye safu ya ushambuliaji.
Simba ina kazi ya kuanza kusaka ushindi kwenye mchezo wa kwanza ugenini nchini Nigeria mchezo unaotarajiwa kuchezwa kati ya Novemba 27-29, mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Desemba 4-6.
Sven amesema kuwa wanakutana na timu bora hasa kwenye safu ya ushambuliaji jambo ambalo linawafanya waichukulie kwa uzito mkubwa mechi hiyo.
Kocha huyo raia wa Ubelgiji amesema:”Ukiwa unakutana na mpinzani ambaye ni mzuri kwenye safu ya ushambuliaji hapo ni muhimu kuongeza nguvu hasa kwenye ulinzi ili kutoruhusu kufungwa, ninawajua wapinzani wetu hiyo tutajipanga kufanya vizuri,” amesema.
Kocha endelea kuandaa vyema vijana, tutafika mbali zaidi ya Ile aliyotufikisha kocha wetu kabla yako Patrick. Nguvu,Ari,nia na uwezo tunao 🤝 tutafika *sisi ndo wawakilishi wa Tanzania tunafamilia kubwa nyuma yetu inatutegemea tuwabebe nao mwakani wapande ndege* nguvu yakujitegemea kupata tiketi ya ushiriki hawana wanatutegemea. Simba oyeeee! 💪 Nguvu moja mbele kwa mbele hadi kilele...
ReplyDelete