November 27, 2020


 IMEELEZWA kuwa aliyekuwa Kocha Mkuu wa Namungo FC, Hitimana Thiery yupo kwenye hesabu za kuibukia ndani ya Klabu ya Mtibwa Sugar ambayo kwa sasa ina Kaimu Kocha Mkuu.


Mtibwa Sugar ilikuwa inanolewa na Zuber Katwila ambaye alibwaga manyanga na kuibukia ndani ya kikosi cha Ihefu ya Mbeya na nafasi yake ikawa chini ya Kocha Msaidizi Vincent Barnaba.


Namungo ilimchimbisha Thiery kutokana na mwendo mbovu ndani ya timu hiyo na mikoba yake ipo mikononi mwa Hemed Morroco.

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa kuna pengo kubwa kwa upande wa benchi la ufundi hivyo kinachofanyika kwa wakati huu ni kupitia CV za makocha ambao wameomba kazi.


"Kuna pengo kubwa hasa kwenye benchi la ufundi kinachofanyika kwa sasa ni kupitia CV za makocha ambao wameomba nafasi ya kufundisha kisha baada ya hapo tutaweka kila kitu wazi.


"Barua ni nyingi zimekuja ukizingatia kwamba Mtibwa Sugar ni taasisi kubwa kuhusu Hitimana bado haijawa rasmi kama anaweza kuja kufundisha hapa," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic