November 8, 2020




Na Mwandishi Wetu, Port Elizabeth 

Kikosi cha timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania chini ya miaka 17 kinacheza mechi yake ya tatu ya michuano ya Cosafa leo jijini Port Elizabeth.

Mechi hiyo ni dhidi ya wenyeji Afrika Kusini na inakua ni sawa na fainali kwa kuwa kama wakipoteza leo basi watakuwa wameaga mashindano kwa asilimia 90.

Wanachotakiwa ni kushinda leo dhidi ya wenyeji ili mechi ya mwisho dhidi ya Zimbabwe hata sare itakuwa ni sahihi kusonga.

Tayari Tanzania imecheza mechi mbili dhidi ya Comoro na kushinda 5-1 na mechi ya pili wakipoteza 2-1 dhidi ya Zambia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic