November 16, 2020



PAUL Pogba kiungo wa Klabu ya Manchester United huenda akaibukia ndani ya Klabu ya Real Madrid msimu ujao kutokana na kutopewa nafasi ndani ya kikosi cha kwanza.

Nyota huyo ambaye anacheza timu ya Taifa ya Ufaransa ndani ya United inayonolewa na Kocha Mkuu Ole Gunnar Solskaer amekuwa haanzi kikosi cha kwanza na badala yake Bruno Fernandes amekuwa akianza.

Nyota huyo mwenye miaka 27 hakuwa kwenye mpango wa Ole kwenye mechi mbili mfululizo ambapo ilikuwa mbele ya Istanbul Basaksehir na Everton Uwanja wa Goodson Park jambo ambalo linaongeza nguvu ya yeye kuondoka kwa kuwa aliweka wazi kuwa anahitaji kupata changamoto mpya. 

Pogba mwenye miaka 27 aliweka bayana kuwa ndoto yake ni kucheza kwenye Ligi ya Hispania kwa kuwa anaamini ina ushindani mkubwa huku timu anayopenda ni Madrid.


"Kwenye maisha ya soka kila mtu anapenda changamoto mpya na mimi ni mchezaji pia, nina ndoto ya siku moja ya kucheza ndani ya Real Madrid, kwa nini hapana siku moja?


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic