November 16, 2020


NYOTA mpya wa Yanga,  Said Ntibazonkiza raia wa Burundi amezidi kuwasha moto kwenye timu yake ya Taifa kwa kufunga mabao muhimu ya ushindi kwenye timu yake.


Ntibazonkiza ambaye ni mshambuliaji amekuwa kwenye mwendelezo bora wa kucheka na nyavu kwenye mechi zake mbili mfululizo alizocheza za kuwania kufuzu Afcon itakayofanyika nchini Cameroon.


Kwenye mchezo wa jana, Novemba 15, Burundi ilishinda kwa mabao 3-1 dhidi ya Mauritania na nyota huyo mali ya Yanga alifunga mabao mawili, moja kwa mpira wa adhabu nje kidogo ya 18 na lile la pili alifunga ndani ya 18.


Kwa idadi hiyo anakuwa amewafunga Mauritania mabao matatu, moja aliwafunga kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Novemba 11.

Mchezo wao ujao ni dhidi ya Central African Republic Novemba 22 na Burundi watakuwa nyumbani. 

Burundi ikiwa kundi E imecheza mechi nne, imeshinda moja, sare moja na kupoteza mechi mbili ikiwa na pointi nne kibindoni na vinara ni Morocco wenye pointi saba. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic