TIMU ya Manchester United imepata hofu kuhusiana na tabia ya kinda wao Mason Greenwood kuonekana kupenda kujirusha kuliko kupumzika.
Klabu hiyo imesema kuwa kuna hofu kubwa kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 19 amekuwa akibadilika tabia kila siku na sasa hapati muda wa kutosha wa kulala.
Inaelezwa kuwa kinda huyo ni mtoto wa bata sana hali ambayo inamyima nafasi ya kutosha kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu England.
Hivi karibuni imekuwa ikiripotiwa kuwa staa huyo amekuwa akishindwa kufanya vizuri mazoezini.
Hata hivyo, habari zinasema kuwa kocha wa timu hiyo Ole Gunnar Solkjaer, amesema kuwa anataka kupambana naye ili arudi kwenye kasi yake.
Ameanza kuwa na tabia mbovu kuanzia alipoondolewa kwenye kambi ya timu ya taifa ya England kutokana na kumuingiza mwanamke kwenye vyumba vya kambi ya taifa.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka Mirror Footbal imeeleza kuwa mashabiki wanahofia uwezo wa nyota huyo unaweza kushuka mithili ya Ravel Morrison mwenye miaka 27 ambaye aliwahi kucheza ndani ya timu hiyo.
Morrison???!!?
ReplyDelete