MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Manchester City, Raheem Sterling ana matumaini ya kuanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Tottenham baada ya kupata majeraha akiwa kwenye mazoezi na timu ya Taifa ya England.
Sterling aliumia wakati timu yake ikiwa kwenye maandalizi ya mchezo dhidi ya Ubelgiji uliochezwa jana Novemba 15 na timu yake kupoteza kwa kufungwa mabao 2-0.
Manchester City chini ya Pep Guardiola ina kazi ya kukutana na Tottenham ya Kocha Mkuu, Jose Mourinho Novemba 20 ikiwa imetoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Liverpool, Novemba 8.
Pia nyota huyo anaweza kuukosa mchezo wa Jumatano, Novemba 18 kwa timu yake ya Taifa dhidi ya Iceland Uwanja wa Wembley, kuanza kwake itategemea maamuzi ya kocha wake Gareth Southgate.
Ripoti zinaeleza kuwa maumivu aliyopata siyo makubwa sana jambo ambalo linatoa nafasi kwake kuanza kwenye mchezo dhidi ya Tottenham.
0 COMMENTS:
Post a Comment