November 16, 2020


MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji amesema kuwa hela zote za usajili yeye anatoa kwa kuwa timu hiyo haina hela.

Jana, Novemba 15 Dewji alizungumza na Waandishi wa Habari na kuweka bayana mpango wa timu hiyo ni kufika mbali kimataifa.

Dewji ameweka wazi kuwa miongoni mwa wachezaji ambao ametoa pesa zake na kuwasajili ni pamoja na kiungo mshambuliaji Luis Miquissone pamoja Clatous Chama.

Suala la Chama lilivuta hisia za wengi ambapo habari zilikuwa zinaeleza kuwa yupo kwenye rada za Yanga jambo ambalo ameliweka wazi kwa kusema kuwa nyota huyo ana mkataba na Simba mpaka 2022.

Dewji amesema:-"Bado hatujaandaa bajeti ya usajili, hivi sasa tunasubiria mapendekezo ya wachezaji ambao kocha anawahitaji, lakini Simba haina hela ila mimi ndio natoa hela.


"Katika hilo la usajili nimepanga kuja na utaratibu mpya wa usajili wa wachezaji wetu kwa kuwapa mikataba mirefu kwa kuanzia miaka minne kwenda mbele," amesema.


7 COMMENTS:

  1. Mwandishi mjinga haswa.Alichokisema Dewji mi kwamba anaongezea deficit ya bilioni 3 kila mwaka ili kufidia bajeti ya mwaka. Usichague unachotaka kuandika wewe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mo Dewji alikuwa mubashara na waandishi tulikuwepo mwandishi acha kuchukua angle negative weka mzani aliouweka Mo

      Delete
    2. Bora ata mlikuwepo live mana kwa kugeuza habari hawajambo

      Delete
  2. Ila nadhani ndio maana Muheshimiwa Magufuli ameichukua office ya uwezekezaji kuipeleka kwenye office yake. Ikiwa muekezaji wa ndani mzawa na mwanachama wa muda mrefu wa simba Mohamed amapigwa pigwa Dana dana kukamilisha uwekezaji pale simba vipi muekezaji mgeni? Miaka mitatu sasa Mo anazungushwa Muheshimiwa Raisi unataka timu zetu kushinda ila timu yenye nguvu kiuchumi kuna uwezekano mkubwa kuwa na nguvu uwanjani pia.

    ReplyDelete
  3. Iv mwandsh ana akil kwel maneno yake na kichwa cha abal nitofaut na maneno ya mo mwandsh amuna k2 kchwan au ana fanya midahalo inoge

    ReplyDelete
  4. Ningekua nauwezo ningekudunga likibao muandshi gan mayai

    ReplyDelete
  5. Tusipepese macho, pana ukweli hapo kuwa Simba haina hela. Pili, sio sahihi kama Mo ambaye ni mwekezaji wa ndani anazungushwa bali Mo anaizungusha Simba kulipa 20 bil za kimkataba wa uwekezaji. Umaskini wetu unataka uhalalishe utapeli wa mwekezaji. Tatizo letu sisi wa Tz tunapenda mpira kuliko vilabu vyetu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic