BAADA ya kikosi cha Yanga kumalizana na Simba Novemba 7 Uwanja wa Mkapa kwa sare yakufungana bao 1-1 na wachezaji kupewa mapumziko kesho Novemba 12 wanatarajiwa kurejea kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya African Lyon.
Mchezo huo wa kirafiki unatarajiwa kuchezwa Novemba 15, Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku.
Mchezo huo wa kirafiki ni maalumu kwa ajili ya kukiweka fiti kikosi hicho ambacho kinawania ubingwa wa Ligi Kuu Bara kikiwa nafasi ya pili na pointi 24 .
Hafidh Saleh, Meneja wa Yanga amesema kuwa kila kitu kipo sawa na kesho wanatarajia kuanza maandalizi kwa mchezo huo.
"Kila kitu kipo sawa, wachezaji wataripoti kambini kesho na kuanza maandalizi ya mchezo wetu wa kirafiki, mashabiki wajitokeze kwa wingi," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment