OFISA Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa watapambana kufanya vizuri kwenye mechi zao zijazo ili kupata matokeo chanya.
Ikiwa ipo nafasi ya 12 na pointi zake kibindoni ni 11 inakutana na Tanzania Prisons iliyo nafasi ya nane na pointi zake ni 15.
Mchezo huo wa ligi unatarajiwa kuchezwa Novemba 21, Uwanja wa Nelson Mandela saa 8:00 mchana.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kifaru amesema:"Tupo vizuri wachezaji wanauwezo mkubwa wa kutafuta matokeo na kila mmoja anatambua kwamba tunahitaji kufanya vizuri.
"Matokeo ndani ya uwanja huwa yanakuja kwa njia tofauti lakini tupo tayari kuleta ushindani ukizingatia kwamba timu yetu ni ya muda mrefu na ina historia nzuri.
"Usisahau kwamba tuliwafunga Azam FC wale ambao walikuwa hawajafungwa kwa muda sasa sisi tuiwatuliza kwa kuwa awali walikuwa wanakutana na timu ndogo, sisi ni timu kubwa na tutapambana kufanya makubwa," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment