November 28, 2020




 NDANI ya uwanja msimu huu wa 2020/21, kiungo wa Yanga, Carlos Carlinhos, amemfunika vibaya Bernard Morrison wa Simba.

 

Simba ikiwa imecheza mechi 11, Morrison ametumika mechi nane akikosekana tatu ambapo alikuwa akitumikia adhabu ya kufungiwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kutokana na kosa la kumpiga ngumi beki wa Ruvu Shooting, Juma Nyosso.

 

Mghana huyo ametumia dakika 419 uwanjani akiwa na Simba na ana hatari kila baada ya dakika 139. Morrison aliyewahi kuichezea Yanga kabla ya kutua Simba, amehusika kwenye mabao matatu kati ya 29 yaliyofungwa na timu hiyo msimu huu kwenye Ligi Kuu Bara akiwa amefunga moja na kutoa pasi mbili za mabao.

 

Rekodi hizo za Morrison, zimemezwa jumla na nyota wa Yanga, Carlinhos ambaye amehusika kwenye mabao manne kati ya 14 yaliyofungwa na timu yake.

 

Carlinhos amefunga mabao mawili yote akifunga kwa kichwa na ametengeneza pasi mbili za mabao yaliyofungwa na nahodha wake, Lamine Moro.

 

Akiwa amecheza mechi tano, raia huyo wa Angola ametumia dakika 317 akiwa na hatari ndani ya uwanja kila baada ya dakika 79 na hajawahi kufungiwa na TPLB kutokana na nidhamu yake kuwa nzuri licha ya kuwa ni miongoni mwa wachezaji wanaochezewa faulo nyingi ndani ya uwanja.



 

Mechi na dakika za Morrison: Ihefu FC (DK 67), Mtibwa Sugar (DK 66), Biashara United (DK 25), Gwambina (DK 23), JKT Tanzania (DK 13), Prisons (DK 90), Ruvu Shooting (DK 45) na Coastal Union (DK 90). Kwa upande wa Carlinhos, mechi na dakika zake ni: Mbeya City (DK 30), Kagera Sugar (DK 35), Mtibwa Sugar (DK 72), Coastal Union (DK 90).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic