KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroek, amesema beki wa timu hiyo, Gadiel Michael amepata matatizo ya kifamilia jambo ambalo linamfanya akosekane ndani ya kikosi.
Gadiel amekuwa akikaa benchi kwa muda mrefu baada ya nafasi yake kuchezwa na Mohammed Hussein ambaye ni chaguo namba moja la Sven.
Kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex kwenye sare ya bila kufungana Gadiel hakuwepo kwenye kikosi.
Sven amempa:-“Tumempa ruhusa Gadiel kutokana na matatizo ya kifamilia aliyonayo lakini atajiunga na timu hivi karibuni,” amesema Sven.
Leo Simba ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Coastal Union kwenye mchezo wa ligi utakaochezwa Uwanja wa Sheik Amri Abeid.
Huu ujinga wa kuripoti hsbari wiki mbili baada ya Gadiel kuomba ruhusa ni matokeo ya ukanjanja wa kutofanya follow up.
ReplyDeleteGadiel yupo Arusha na timu.
Aliyeandika habari hii sijui aliwaza nini?
Mwandishi ni mwonho sana.
Delete