November 14, 2020

 


TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imebanwa mbavu na kikosi cha Tunisia kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2022 nchini Cameroon.


Bao pekee la ushindi kwa Tunisia, kwenye mchezo wa kundi J uliochezwa Novemba 13 limefungwa na Youssel Msakni dakika ya 18 kwa mkwaju wa penalti.


Jitihada za Stras kupata bao zimekuwa ngumu usiku wa kuamkia leo nchini Tunisa kwa kubanwa mbavu mpaka dakika 90 kukamilika.


Nyota wawili wa Stars, Simon Msuva na Bakari Mwamnyeto walionyeshwa kadi ya njano kwenye mchezo huo ambao Tunisia waliutawala kwa kiasi kikubwa eneo la kiungo na ushambuliaji huku Aishi Manula akifanya kazi ya ziada kuokoa michomo minne ya hatari kipindi cha pili.


Bakari Mwamnyeto, Erasto Nyoni na Shomari Kapombe mabeki wa Stars pamoja na Mohamed Hussein walikuwa na kazi ya kufanya kwa kuwa washambuliaji wa Sudan walikuwa wakiweka ngome lango la Manula.


John Bocco na Msuva walikuwa wakipata tabu mbele kwa kuwa ilikuwa ikiwalazimu kurudi nyuma kuokoa mashambulizi na kutengeneza nafasi za kwenda kufunga jambo ambalo limewafanya washindwe kufanya hatari kwa Tunisia.


Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Novemba 17, Uwanja wa Mkapa.

12 COMMENTS:

  1. Yakhe,tumewaweza, sasa tunakuja kuwalamba 2 bila

    ReplyDelete
  2. S.jembe tuna wasiwasi na elimu yako broo!unaenda nje ya box mara nying mno

    ReplyDelete
  3. Wamejitahid sasa Hao tunis 17 nov tuwachezeshe saa 9 alasir jua la utos watakaa 4 kw mkapa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaani, hata saa saba mchana ingewezekana tuwachezeshe. Ila nimeona tangazo azam tv kuwa mechi ijayo na Tunisia hiyo tarehe 17 itachezwa saa nne usiku. Sjajua kama huo muda tumejipangia wenyewe kama nchi au tumepangiwa na CAF

      Delete
  4. Mwandishi hauko siriazi, ni Tunisia au Sudan?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yan kaandika utafikiri alikuwa anakimbizwa..Nadhan hii blog imejaa waandishi waliokosa umakini. Makosa yamekuwa mengi sana katika habari zao

      Delete
  5. Nawapongeza sana wachezaji Wa stars maana wale watunisia wako vizuri fiziki na hata ubunifu shukrani za pekee kwa Aishi Manila na beki zake kwa kujitahidi kulinda lango lao vyema maana hata penalty waliyopewa ilikuwa sio Kali kivile

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli kabisa. Tumejitahidi sanaaa na wapiganaji wetu walijitoa kweli kweli ,Kama sio hivyo tungepigwa nyingi.

      Delete
  6. Tatizo kazoea stori za kutunga

    ReplyDelete
  7. star ad xaiv ina tia moyo mpaka apo wakija bongo n kpgo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic