November 11, 2020


 IMEELEZWA kuwa uongozi wa Simba upo kwenye mchakato wa kuongeza kiungo mkabaji ndani ya timu hiyo ambayo inaiwakilisha Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu wa 2020/21 na itaanza kibarua chake kati ya Novemba 27-29.


Simba imepangwa kucheza na Klabu ya Plateu United kutoka Nigeria mchezo wa kwanza itakuwa ugenini na ule wa pili utachezwa Uwanja wa Mkapa kati ya Desemba 4-6.

Kwa sasa mabingwa hao watetezi kwenye nafasi ya kiungo mkabaji wanamtumia Jonas Mkude, Said Ndemla na Mzamiru Yassin huku wakiikosa huduma ya raia wa Brazil, Gerson Fraga ambaye atakuwa nje kwa msimu mzima.


Nyota anayetajwa kurejeshwa kundini ni James Kotei ambaye ana tuzo ya mchezaji bora ndani ya Simba kwa upande wa viungo aliyoitwaa msimu wa 2018/19 kwenye tuzo za Mo Award.


Pia kwenye mchakato wa kuachwa kwa kiungo huyo ambaye alitimkia Afrika Kusini kuliibuka mvutano mkubwa kabla hajasajiliwa na Klabu ya Kaizer Chief na kwa sasa yupo zake FC Slavia anapewa nafasi ya kurejea tena.


"Kwa sasa Simba ipo kwenye mpango wa kumrejesha kiungo wao mkata umeme  namba moja, Kotei, (James) ambaye wakati anaondoka bado kocha alikuwa anahitaji huduma yake," ilieleza taarifa hiyo.


Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba ameweka bayana kuwa wanahitaji umakini katika kusaka ushindi kwenye mechi zao za Ligi ya Mabingwa Afrika.

21 COMMENTS:

  1. Wanalamba matapishi. Sikinde waliimba talaka ya hasira na ukiambiwa uangukie unatoa pesa nyingi. Sasa ni zamu yake kuringa

    ReplyDelete
  2. Mimi kinachonishangaza na kwa kiasi fulani kinakera ni kwamba simba hatuna uwezo wa kutafuta kiungo bora zaidi kuliko kotei? Miaka nenda rudi kotei,kotei,Kotei. Ikiwa Yanga hawapo hata kwenye mashindano ya kimataifa wamejitutumua kwenda kuchukua wachezaji vita club na simba Tunajua uwezo wa Tonombe kama kiungo mkabaji yupo juu kuliko kotei sio siri. Tatizo la kiungo mkabaji simba wa kwenda kupigana vita ya klabu bingwa Africa bado hatuna simba na ni donda ndugu na ndio kitu kitachokwenda kutuangusha kwenye Klabu bingwa Africa hata mara hii kama viongozi hawataamua kuacha mzaha na kuwa serious kutafuta mtu wa kazi kweli kweli wa kuja kuimarisha ulinzi kwenye kiungo cha chini.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuna watu hawataki kuuona ukweli huu

      Delete
    2. Sidhani Kotei ni mbadala muafaka wa Fraga.Na hata Okwi anayepigiwa chapuo kurudi Msimbazi ni upuuzi mtupu hasa ukiangalia umri wake.Kunahitajika viungo mkabaji mwenye nguvu, control ability na speed.Simba waweke fungu la maana Kwa wachezaji wa viwango hivyo na sio kuvizia vizia scouting ya Yanga.Kuna kiungo mkabaji mzuri mu-ivory coast pale TP Mazembe ambaye aliwahi kufanya majaribio Simba chini ya Aussems.Nina wasiwasi na timu yetu ya Simba bado inacheza mpira laini.Na hata hawa majeruhi wa mara Kwa mara kina Bocco, Kagere nao wanatakiwa kutafutiwa mbadala kama kina Mukusu.Viongozi wa Simba kuweni serious na usajili wa kuleta tija na sio kufikiria kuikomoa Yanga.

      Delete
    3. ww mwiko kusema maneno haya.
      utafikishwa polisi, tangulini simba ikawa donda ndugu, ina wachezaji wengi wazuri na ndio klabu bora Tz, sasa kuifananisha na Yanga ni sawa na kumfananisha bilgeth na diamond. usirudie tena, Simba level zake ni Al Ahyl

      Delete
    4. Jair ame sema ukwel maana uki zingatia viongoz wa simb wana penda sana kuludia wachezaji wale wale kwamb hakuna viungo kwenye tim kubwa kubwa wana taja kina kotei kwamb akuna wachezaj wengne ata as vta tp mazembe nkana na zngnezo wana leta kwanza kina falaga ata nguvu hawana smb ina takiwa iwe silias

      Delete
  3. Kotei mtambo, ukirejea mwakemwake. GSM walitapatapa wakachemka wakamsajili garasa laburundi kutoka vitalo.

    ReplyDelete
  4. ONESHENI ULIMWENGU KUA MNA URAFIKI NA AL AHLI MPEWE KWA MKOPO KIUNGO MKABAJI MMOJA

    ReplyDelete
  5. Kwani hakuna viungo wazuri si wapo wamejaa kuliko kurudisha wachezaji walio achwa ni akili ama ujinga? Hatufiki kokote kwa ujinga huu hata kombe hatuchukuwi la ligi tusahau kuna ujinga wa viongozi ndani ya timu MO anatowa pesa zake watu wanakula watuharibie timu inauma sana

    ReplyDelete
  6. Hii simba inachekesha kwanini wasisajili kutokana na matakwa ya timu halafu wanaangaika utafikiri wachezaji wameisha kumbe wapo wengi tena tena wa bei nafuu

    ReplyDelete
  7. ona sasa akili mbovu kwani hao viungo wa bongo hawafundishiki yaani mnawarate vipi ina maana hata uko Taifa Stars mnajua hawana cha kutusaidia yaani wamekuwa mbwa wazeee kabisaaaa kufuata maelekezo wakawa wazuri au afadhali. Mi naona hamna maslahi na soka letu na ni wabinafsi sanaa mikia nyie

    ReplyDelete
    Replies
    1. Heee vipi povu mbona Yanga ina kina Mukoko inakuwaje inakuuma Kwa Simba?

      Delete
  8. Yani kweli mikia fc mtabaki kuwa mikia tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kabisa Yani kotei Tena?ndo shida ya mikia fc wanachemka shauri ya yanga,wanaiofia yanga adi wanasajili kwa kuangalia yanga,kumbe wanaingia chaka

      Delete
  9. Hii ni story ya kutunga ya mwandishi huyu

    ReplyDelete
  10. Mukoko Tunombe atatufaa siku zijazo.

    ReplyDelete
  11. simba wanamleta Makusu kuwatungua Yanga magoli 5 round ya pili

    ReplyDelete
  12. Simba mashoga kweli nawaambia tena na bado mpaka mtapigana viongozi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha matusi wewe 🤫, funga Domo Kama huna point.

      Delete
  13. Hakuna kitu kama hicho. Kotei arudi Simba kwa kiwango gani? Acheni kutunga stori.

    ReplyDelete
  14. Kwanza mwandsh wa mwaka huyu ana tunga stol kama ame toka ofice za komedian centers

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic