November 11, 2020

 


UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa sasa nyota wao Clatous Chama ataendelea kuwa ndani ya kikosi hicho kwa kuwa ni mali yao.


Chama mwenye mabao mawili ndani ya Ligi Kuu Bara na pasi tano kwa msimu wa 2020/21 kati ya mabao 22 yaliyofungwa na Simba anatajwa kuingia kwenye rada za watani wa jadi Yanga.


Kwenye wakati wa usajili wa dirisha kubwa msimu uliopita, Fredrick Mwakalebela ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Yanga alisema kuwa wamefanya mazungumzo na kiungo huyo.


Baadaye alikanusha taarifa hizo baada ya uongozi wa Simba kumjibu na kupeleka malalamiko Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) kwa kuwa Yanga ilikiuka vigezo vya usajili wa mchezaji kwa mujibu wa Fifa kwa kuzungumza na mchezaji ambaye bado ana mkataba.


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa Chama ni mali ya timu hiyo na hakuna mpango wa yeye kuibukia timu nyingine kwa sasa.


"Hizo ni habari tu ambazo zinaeleza kwamba Chama anaondoka anakwenda sijui wapi, lakini ukweli ni kwamba mwamba bado yupo ndani ya Simba na suala la kuondoka bado sana.


"Kwa sasa akili zetu tumeziwekeza kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kisha mambo hayo mengine yatafuata," amesema.


Simba inawakilisha nchi kwenye Ligi ya Mabingwa ambapo ina kazi ya kusaka ushindi mbele ya Plateu United ya Nigeria.


Mchezo wa kwanza kwa Simba unatarajiwa kuwa nchini Nigeria Uwanja wa Jos kati ya Novemba 27-29 na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa kati ya Desemba 4-6, Uwanja wa Mkapa.  

5 COMMENTS:

  1. Wanachama wa yanga na washabiki wao wanahangaika sana kuhusu Chama wanamponda huku wanamtaka

    ReplyDelete
    Replies
    1. kama nyie mlivyofanya kwa morison! malipo hapa hapa dunia mazafanta tulieni

      Delete
    2. 😄😄😄😄 Morrison anaendelea na ataendelea kuwakera. Eti mlipe kwa chama wakati sure boy toka Azam mlichemka, shiboub akiwa guru tulimwacha mkachemka.

      Delete
  2. Walimtaka Sure Boy kwa bei chee hawakumpata vipi muweze kumtowa Chama Kutoka kwa Moooo au ndio wnafikiri ni mchezaji bei powa Hahaaaa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic