November 11, 2020

 


VINARA wa Ligi Kuu Bara, Azam FC kwa sasa wamerejea chimbo kuivutia kasi Klabu ya KMC kwenye mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara.


Ushindi wao wa mabao 3-0 dhidi Dodoma Jiji unawafanya wawe nafasi ya kwanza na pointi 25 kibindoni wakifuatiwa na Yanga iliyo nafasi ya pili na pointi 24.


Ikiwa imecheza mechi 10 kinara wao wa kutengeneza mabao ni Prince Dube ambaye pia ni mtambo wa mabao akiwa amefunga jumla ya mabao sita na ana pasi nne za mabao.


Kikosi hicho baada ya mapumziko ya siku tatu kilirejea rasmi kwenye maandalizi ya mechi zao Jumatatu, Novemba 8 kikiwa chini ya Kocha Mkuu, Arstica Cioaba.


Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa maandalizi mazuri ni muhimu kwa timu hiyo ili iweze kufikia malengo iliyojiwekea.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic