ADAM Adam mshambuliaji anayeongoza kwa mabao kwa upande wa wazawa katika Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa nayo 6 hakuambatana na timu ya Taifa ya Tanzania nchini Uturuki kutokana na kukosa pasi (Passport) ya kusafiria.
Pia Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta anayeichezea Klabu ya FC Fenerbahce ya Uturuki nae atakosekana katika kikosi cha Stars kitakachocheza michezo ya kufuzu Afcon 2021 dhidi ya Tunisia Novemba 13 (Tunisia) na Novemba 16 (Dar) baada ya kushauriwa na madaktari wa klabu yake kupumzika kwa siku 10 kutokana na kuwa na tatizo la kiafya
Stars ambayo ilikuwa imeweka kambi kwa muda wa siku tatu Instabul leo imeanza safari ya kuelekea Tunisia kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo ambao utachezwa nchini Tunisia.
Kocha Mkuu wa Stars, Ettiene Ndayiragije amesema kuwa wachezaji wapo vizuri ila watakosa huduma ya Samatta ambaye anapaswa kupumzika kwa muda wa wiki mbili.
"Wengine wapo ambao watacheza nafasi yake na itakuwa ni faraja kwake kuona tukipata ushindi," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment