November 12, 2020


UONGOZI wa Klabu ya Yanga umesema kuwa hauna presha na mambo yote ambayo yanaendelea ndani ya Bongo kwa kuwa wamejipanga kufanya vema kwa msimu wa 2020/21.


Kwa sasa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 24 baada ya kucheza mechi 10 na imefunga jumla ya mabao 12 huku safu ya ulinzi ikiruhusu mabao matatu.


Kaze alipokea mikoba kutoka kwa Zlatko Krmpotic ambaye alikiongoza kikosi kwenye mechi tano ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons,Mbeya City, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar na Coastal Union.


Kwenye Dar, Dabi iliyochezwa Novemba 7, Uwanja wa Mkapa wakati wakitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 bao la Yanga lilipatikana kwa penalti ambayo imekuwa ikilalamikiwa na mashabiki wa Simba wakidai kuwa haikuwa halali. 


Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa wamekuwa wakiwekewa vikwazo na baadhi ya watu ambao wanawaombea mabaya jambo ambalo haliwapi presha.


"Wapo ambao wanatuombea mabaya ili kuona kwamba hatufikii mafanikio yetu katika hilo halitupi mashaka tutaendelea kuwa imara na kupambana kufikia malengo yetu.


"Kila kitu kipo sawa ninawaambia mashabiki kwamba waendelee kuipa sapoti timu yao bila kukata tamaa hii ni timu ya Wananchi na kila shabiki anapaswa kuifurahia timu yake," amesema.


Novemba 15, Yanga inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya African Lyon unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic