ZINADINE Zidane, Kocha Mkuu wa Real Madrid amesema kuwa alipata bahati ya kuzungumza na Diego Maradona na alimwambia kwambe yeye ni aina ya wachezaji bora ndani ya uwanja.
Zidane amesema kuwa taarifa za kutangulia mbele za haki kwa gwiji huyo zilimshtua na kumfanya afikirie mambo mengi kuhusu uwezo wa Maradona.
Maradona alitangulia mbele za haki Novemba 25 akiwa nyumbani, Argentina ikiwa ni muda mfupi baada ya kutimiza miaka 60.
Zidane amesema:"Hakuwa mtu mwenye maneno mengi ila utendaji zaidi, nilipata bahati ya kuzungumza naye na nilimuambia kwamba yeye ni mchezaji bora na mwenye uwezo ndani ya uwanja.
"Kwa kuwa ametangulia basi hakuna namna imani ni kwamba uwezo wake utadumu kwenye mioyo ya wanafamilia ya michezo," .
ni kwwli kabisa, nakumbuka tarehe 24novemba nilipochukua kiatu cha maradona mara baada ya kumaliza mchezo wa kombe la mataifa kipindi kile,
ReplyDeletemaradona aliamua mechi ile kwa ubabe n kuipelea Argentina fainali.
Nikiwa jukwaani Argentina niliamini "football is not a positive fair play"