December 6, 2020


 IKIWA leo Yanga inashuka Uwanja wa Mkapa kumenyana na Ruvu Shooting Uwanja wa Mkapa, nyota wawili wataukosa mchezo wa leo huku wawili wengine hatma yao ikiwa mikononi mwa Kocha Mkuu Cedric Kaze.


Yanga ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 31 inakutana na Ruvu Shooting iliyo nafasi ya nne na pointi 23 zote zimecheza mechi 13.


Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo wa leo huku nyota wawili ambao walikuwa wanasumbuliwa na majeraha baada ya kuukosa mchezo wa ligi dhidi ya JKT Tanzania wanaweza kuanza ikiwa mwalimu atawahitaji.

"Lamine Moro na Shomari Kibwana wapo tayari kwa ajili ya mchezo hivyo mwalimu anaweza kuwatumia akiwahitaji.

"Carlos Carlinhos yeye anasumbuliwa na nyonga hivyo ataukosa mchezo wa leo dhidi ya Ruvu Shooting," amesema.


Nyota mwingine ambaye atakosekana ni Mapinduzi Balama ambaye amekwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa matibabu zaidi ya mguu aliopata msimu uliopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic