December 29, 2020


 BEKI wa zamani wa Klabu ya Simba, Juuko Murshid amepata dili la kujiunga na Klabu ya Maritzburg United cha Afrika Kusini.

Beki huyo kitasa kipenzi cha mashabiki wa Simba raia wa Uganda alikipiga ndani ya Simba msimu wa 2014-19 ambapo alikuwa ni chaguo namba moja kikosi cha kwanza.

Rekodi zinaonyesha kwamba alicheza jumla ya mechi 149 na kutupia mabao 7 licha ya kwamba ni beki.

Alisepa Simba na kuwa ndani ya kikosi cha Wydad ya na kwa sasa yupo zake nchini Uganda.


Taarifa iliyotolewa na Klabu Express ya Uganda imeeleza kuwa nyota huyo amepata dili la kwenda kufanya majaribio nchini Afrika Kusini kwa muda wa wiki moja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic