December 29, 2020


 KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji amecharuka na kuwataka wachezaji wake kucheza kwa kujituma kuelekea kwenye mchezo wa marudio wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum.

Simba ilipoteza mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya FC Platinum uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe kwa kufungwa bao 1-0 lililopachikwa na Perfeck Chikwende.

Ina kibarua cha kupindua meza Uwanja wa Mkapa unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Januari 6, ambapo Ofisa Habari wa timu hiyo Haji Manara amesema kuwa utakuwa ni mchezo wa vita ndani ya Dar.

Vandenbroeck amesema kuwa kilichowaponza washindwe kushinda mchezo huo ni kukosekana kwa umakini kwa wachezaji wake jambo ambalo limemkasirisha hasa hivyo hatapenda kuona makosa yanajirudia.


“Tuliweka wazi malengo yetu tangu awali kwamba ni lazima tuweze kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika. Kuanza kwa kupoteza hiyo ni mbaya kwetu na haijanifurahisha hasa kwa kuwa mchezo tuliweza kuumiliki ila umakini ulikosekana.

“Kwenye mchezo wetu wa marudio hatuna chaguo la kufanya zaidi ya kutafuta matokeo chanya na wachezaji kujituma zaidi, hivyo mashabiki watupe sapoti tunaamini kwamba tutafanya vizuri,” amesema Vandenbr.oeck.

3 COMMENTS:

  1. Hatuna kocha hapo kati ya watumishi hewa huyo naye yumo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jaribu kuheshimu mchango wake japo huo mdogo

      Delete
    2. Wengine ni kulaumu. Kocha ambaye amekuwa mataji matatu mwaka mmoja si kocha. Tatizo sisi tunaka tushinde Kila wakati. Acheni maneno ya ovyo. Yupi kocha mzuri Simba. Kama mzuri amabaki miaka mingapi Simba. Miye tangu nishabikiye Simba tangu 1973. Siwezi kujieleza idadi ya makocha waliifundolisha simba.hii ina Manisha kocha hawezi kuifundisha miaka nenda Rudi bila kushindwa. Lazima tuangaliye pia quality ya wachezaki wetu pia. Leteni kocha ambaye hatalaumiwa. Aussems haubaki hata miaka miwili. Omog kivo hivo. Kibadeni kaifkkisha Simba fainali za Caf confederation naye siyo kocha mzuri Yuko wapi. Mashabiki bwana.wakati mwengine tunabwajabwaja tu.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic