ABDI Banda, nyota wa zamani wa Klabu ya Simba ambaye alisajiliwa na kikosi hicho msimu wa 2014 akitokea Klabu ya Coastal Union ya Tanga, amesema kuwa yupo tayari kusaini Simba ikiwa atapewa ofa nzuri kwa kuwa ni timu ambayo inafanikisha malengo ya wachezaji wengi.
Banda alisepa Bongo msimu wa 2017 na kujiunga na Klabu ya Baroka FC ya Afrika Kusini aliyodumu huko mpaka msimu wa 2019 na rekodi zinaonyesha kuwa alicheza jumla ya mechi 41 na alifunga mabao manne.
Beki huyo mzawa aliisajiliwa na Klabu ya Highlands Parks ya Afrika Kusini ambayo kwa sasa imeuzwa na kumfanya aache majukumu ya kurudi kwenye timu hiyo mikononi mwa wakala wake na kwa sasa yupo zake Bongo.
Banda amesema:”Ikiwa itatokea nikahitaji timu ya kusaini kwa Bongo, kipaumbele changu cha kwanza ni Simba ukizingatia kwamba ni timu ambayo imenitoa na kunifanya nifikie hapa nilipo, ninajua kwamba wengi wanapenda kusaini Simba.
“Ikiwa nitapata ofa nyingi, kipaumbele changu nitaanza na Simba lakini kitu cha msingi ni maslahi, Simba ni daraja ambalo linawapitisha wengi hata wakiondoka huwa wanakumbuka yale ambayo wamepitia,” .
Kwa hiyo simba watabugi. Hana uwezo kea sasa, na umri pia.
ReplyDeleteBanda ana umri gan mpka sasa achen izo kuna watu washaanza kucheza kabla y Banda.na bado wanacheza mpka leo we unasema Banda.umri kwan kakaa miaka mingap sauzi
ReplyDeleteAtacheza nafasi gani ikiwa kuna watu wana uwezo mkubwa kuliko yeye na bado wanasugua benchi sembuse yeye
ReplyDeleteHskuna sababu ya kuongeza wachezaji wenye umri mkubea ili hali uwezo wao ni sawa na waliopo. Ili kuwa na mwendelezo sajilini vijana wenye uwezo ambao watakaa muda mrefu au watauzwa na timu kupata mapato sio hao akina banda, okwi kotei
ReplyDeleteBanda amezidi ni miaka 27 sasa hapo kwa umri gani mkubwa kuliko Wawa.....!? Tusijue saana tutaharibu....
DeleteAliondoka kwa maneno machafu sana wakati mwìngine akumbuke kuweka akiba ya maneno
ReplyDeleteHana lolote huyo hamjaona wachezaji wazuri mkachukuwe huyo garasa? Wa nini huyo?
ReplyDeletehuyu jamaa aliondoka kwa dharau sana simba sanaa tu kisa ilikuwa haina hela,kama vile kessy,singano..siyo w akurudisha hawa bor mumrudishe juma nyosso kama mko desperate kiasi hiko
ReplyDeleteHuo ni utunzi wa mwandishi
ReplyDeleteHapo sasa pagumu. Kumbe aliondoka kwa kukejeli, basi abaki huko huko
ReplyDeletevibaya mno tena katukanana na manara kipindi hiko simba mshahara shoda ndugu alivyoenda baroka aliongea shit sana hatujasahau
DeleteSasa hivi simba wasisajili mchezaji ambaye si mchezaji wa timu ya taifa la nchi yake. Tena umri sio zaidi ya 25 years, watu wazima waliopo wanatosha
ReplyDeleteKweli kabisa tunataka vijana kama akina Louis Miquessone na sio kujaza wahenga, hao waliopo wanatosha.
ReplyDeleteAisee aisee aisee acha utani basi akubali kusaini kwani simba wamemfuata andika vizuri bana
ReplyDeleteMikia fc kweli sasa ni kituo cha kulelea wahenga
ReplyDelete