December 6, 2020

 


MCHEZO wa Kombe la Shirikisho kati ya Sudani Kusini na Namungo FC wa marudio kwenye Kombe la Shirikisho ambao ulipaswa uchezwe leo Desemba 6 umefutwa na Caf.


Uamuzi huo umetokana na Chama cha Mpira cha Sudan Kusini (SSFA) kushindwa kukamilisha taratibu kuhusu waamuzi waliopangwa kuchezesha mechi.


Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Namungo ilishinda mabao 3-0 ambapo mawili yalifungwa na Stephen Sey na moja na Shiza Kichuya hivyo leo ilikuwa inahitaji sare ama ishinde ili ipenye hatua ya mtoano.


Kwa kuwa mchezo umefutwa basi Namungo inapeta mpaka hatua ya mtoano Kombe la Shirikisho Afrika.


Taarifa imeeleza namna hii:-


 

6 COMMENTS:

  1. Safi Sana,Namungo fanya maandalizi makubwa sasa

    ReplyDelete
  2. Sasa mbona caf hawajaeleza utafanyika lini tena au namungo ndio ameshapita raund hii

    ReplyDelete
  3. Hii bdo namungo, yaweka record bongo. Ndege bado inawahusu na Simba wote wafuzu kwa cleanshit

    ReplyDelete
  4. Sudan Kusini bado hawako serious na masuala mengi, yaani utaratibu mdogo tu umewashinda,hawa wanaweza kuandaa kombe hata la Africa Mashariki?
    Inaonekana hata usalama si mzuri Bora Namungo hawajaenda

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic