December 16, 2020

 


KOCHA Mkuu wa Manchester City,  Pep Guardiola amesema tatizo kubwa lililopo kwenye timu yake kwa sasa ni ubutu wa washambuliaji wake kushindwa kufunga jambo ambalo linahitaji muda kutafutiwa dawa.

Kocha huyo ameongeza kuwa walikuwa na nafasi ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu England dhidi ya West Brom ila matokeo yake yamekuwa kama yalitokea.

Usiku wa kuamkia leo Manchester City ikiwa Uwanja wa Etihad ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na West Brom na kuwafanya wagawane pointi mojamoja inayowafanya City wafikishe pointi 20 wakiwa nafasi ya sita kwenye mchezo wa Ligi Kuu England. 

Likay Gundogan alipachika bao la kwanza kwa City dakika ya 30 na dakika ya 43 Ruben Dias alijifunga na kuwafanya waende mapumziko wakiwa wametoshana nguvu.

Mpaka dakika 90 zinakamilika timu zote ziligawana pointi mojamoja na kuifanya West Brom kufikisha pointi 7 ikiwa nafasi ya 19.

Guardiola amesema kuwa walimiliki mchezo katika kila kitu ila walishindwa kutumia nafasi ambazo walizipata kipindi cha kwanza na kipindi cha pili jambo lililowafanya washindwe kupata ushindi.


"Tulistahili kushinda kwa kuwa tuliweza kumiliki mchezo. Kwa namna ambavyo tumefanya nadhani tumepiga mashuti 26 ila haikuwa nzuri kwetu hivyo tunapambana kutafuta matokeo," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic