December 16, 2020


 GEORGE Lwandamina, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa wachezaji wake wameonekana kuwa bora ndani ya uwanja jambo analoamini litampa mafanikio kwenye mechi zake zijazo.


Mchezo wake wa kwanza kukaa kwenye benchi akirithi mikoba ya Aristica Cioaba ilikuwa ni Desemba 7 dhidi ya Namungo.


Kwenye mchezo huo alishuhudia vijana wake wakiambulia pointi moja baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.


Lwandamina amesema:"Nimewaona wachezaji ni wazuri, wanacheza kwa kujituma jambo ambalo linaleta matumaini ya kule ambapo tunahitaji kwenda.


"Kupata sare ama kushindwa kulinda ushindi ni sehemu ya matokeo na inatufanya tuanze kujipanga kwa ajili ya mechi zijazo.


"Hakuna mchezaji ambaye amefurahia timu kushindwa kupata ushindi lakini ni somo kwetu wakati ujao kuongeza zaidi juhudi mpaka dakika za mwisho," .


Azam FC ipo nafasi ya tatu ikiwa imecheza jumla ya mechi 15 imekusanya jumla ya pointi 28.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic