LEO Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku, vita kubwa ya kusaka pointi tatu itakuwa ni ya kutoana jasho na damu kwa wakali wa Dar, Simba wenye maskani yao Kariakoo dhidi ya KMC wana Kino Boys.
Jembe jipya la Simba, Thaddeo Lwanga anatarajiwa kuanza leo Uwanja wa Mkapa baada ya kukamilisha masuala ya usajili.
Simba ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck inapambana
kutetea taji la Ligi Kuu Bara huku KMC wao wakihitaji kulipa kisasi cha
kupoteza mchezo wao uliopita kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Pia KMC inakumbuka kwamba mchezo wa mwisho walipokutana na
Simba, ilifungwa mabao 2-0 yote yakifungwa na kiungo mshambuliaji, Luis
Miquissone mwenye jumla ya pasi sita na bao moja kati ya mabao 32.
Mchezo wake uliopita Simba imetoka kushinda bao 1-0 dhidi ya
Mbeya City, ipo nafasi ya pili na pointi 29 inakutana na KMC iliyo nafasi ya
tano na pointi zake ni 21.
Sven Vandenbroek, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa timu zote ndani ya Ligi Kuu Bara ni imara jambo linalomfanya
atafute mbinu za kupata ushindi ndani ya dakika 90.
Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa watawafurahisha mashabiki kwa kushinda kwenye mchezo huo baada ya
kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar.
0 COMMENTS:
Post a Comment