December 16, 2020

 


HITIMANA Thiery aliyekuwa Kocha Mkuu wa Namungo FC anatajwa kuingia kwenye rada za Klabu ya Mtibwa Sugar yenye maskani yake Morogoro.


Habari zinaeleza kuwa baada ya kufutwa ndani ya Namungo kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo amekuwa kwenye mazungumzo na Klabu ya Mtibwa Sugar.

Ikiwa mazungumzo yatakamilika ni suala la muda kwa kocha huyo ambaye ana uzoefu na Ligi Kuu Bara akapewa mikoba ya Zuber Katwila ambaye yupo zake Ihefu FC kwa sasa.

Katwila alisepa ndani ya Mtibwa Sugar na kuibukia Ihefu na kuiacha timu hiyo mikononi mwa kocha msaidizi, Vincent Barnaba.

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa kuna majina ya walimu wengi wanaopenda kuifundisha timu hiyo kutokana na kuwa na misingi imara.

"Hapa Mtibwa Sugar ni chuo na wengi wanapenda kuja kufundisha ndani ya timu hii hivyo mambo yakiwa sawa tutamtangaza yule ambaye atakuja kuwa kocha mkuu ndani ya kikosi chetu.

"Kuhusu Hitimana,(Thiery) kwa sasa sijajua kama ni miongoni mwa wale ambao wameomba kazi ndani ya Mtibwa Sugar, tunaamini tutaweka wazi mambo haya bila tatizo," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic