December 16, 2020


 BAADA ya kufanikiwa kufikisha mabao matatu kwenye Ligi Kuu Bara, kiungo wa Yanga, Deus Kaseke amesema kuwa ataweka jitihada zaidi kila anapopata nafasi ili afunge zaidi na ikiwezekana mwisho wa msimu afikishe mabao 15.

 

Kaseke aliongeza kuwa, kadiri anavyozidi kufunga uwezo wake wa kujiamini unazidi kuongezeka na hiyo inamsaidia yeye katika kuyakimbilia malengo yake ya kutaka kufikisha mabao 15 msimu huu.

 

Kaseke amefunga mabao hayo matatu katika michezo minne aliyocheza hivi karibuni, akifunga bao la ushindi mbele ya Azam FC mchezo ukimalizika kwa Yanga kushinda 1-0 pale Azam Complex, Chamazi, kisha akawapa tena ushindi mbele ya JKT Tanzania, Yanga wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 pale kwa Mkapa na kisha akifunga moja wakati Yanga akishinda 5-0 dhidi ya Mwadui.

 

 Kaseke amesema: “Kwanza nashukuru Mungu kwa kuwa naendelea kupewa nafasi na mwalimu, siyo jambo dogo kucheza mara kwa mara kwenye timu hii ya sasa. Kuhusu kufunga ni ushirikiano kwanza na wenzangu pamoja na jitihada binafsi.

 

“Kufunga mara kwa mara kunaniongezea kujiamini zaidi, nafikiri kama nitakuwa salama hadi mwisho wa msimu, Wanayanga watarajie mabao 15 kutoka kwangu, tuombe Mungu tu.’

1 COMMENTS:

  1. 𝙝𝙖𝙮𝙖 𝙗𝙬𝙖𝙣𝙖 𝙠𝙞𝙡𝙖 𝙡𝙖 𝙠𝙝𝙚𝙧𝙞 𝙬𝙚 𝙤𝙣𝙜𝙚𝙯𝙖 𝙟𝙪𝙝𝙪𝙙𝙞

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic