December 16, 2020

 


SAIDO Ntibanzokiza, nyota mpya wa Yanga amesema kuwa kikosi hicho kinawachezaji wazuri jambo ambalo linamfanya aamini kwamba itakuwa rahisi kufikia malengo.


Nyota huyo ambaye ni ingizo jipya ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Cedric Kaze tayari amefunga mabao mawili ndani ya ardhi ya Bongo akiwa amecheza mchezo mmoja.

Ilikuwa ni jana, Desemba 15 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United wakati timu hiyo ikishinda 3-0.

Ntibanzokiza amesema:"Nimewaona wachezaji wenzangu namna ambavyo wapo na kila mmoja anafanya vizuri ndani ya uwanja hivyo kuna nafasi ya kupata matokeo.

"Kwangu mimi naona kwamba ushirikiano uliopo utatufanya tufikie malengo ambayo tumejiwekea, wakati ni huu na mashabiki wazidi kutupa sapoti," .

Yanga ipo nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 15, imeshinda mechi 11 na kupata sare mechi nne.

Safu yake ya ushambuliaji imefunga mabao 22 huku il ya ulinzi ikiwa imeruhusu mabao matano kwa msimu wa 2020/21.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic