December 12, 2020

 


LEO Desemba 12, Uwanja wa Mo Arena kutakuwa na mchezo wa Dar Dabi kwa Wanawake wenye makazi yao pale Kariakoo ambapo Simba Queens itawakaribisha watani zao wa jadi Yanga Princes.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ambapo makocha wa timu zote mbili wametambiana kusepa na pointi tatu kwenye mchezo wa leo utakaochezwa majira ya saa 10:00 jioni.


Timu zote zimecheza mechi tatu ambapo wenyeji Simba wameshinda mechi mbili na kupata sare moja wakiwa nafasi ya tatu huku Yanga Princes ikiwa imecheza mechi tatu na imeshinda zote kibindoni ina pointi tisa ikiwa nafasi ya kwanza.

Kila timu ikishinda itakuwa imevunja rekodi ya mpinzani wake kwa kuwa ikiwa Simba Queens itashinda leo mbele ya Yanga Princess itavunja rekodi ya Yanga Princess kucheza mechi tatu bila kupoteza. 

Kama Yanga Princess itashinda leo itatibua rekodi ya wapinzani wao Simba Queens kushinda mechi zote nne walipokutana ndani ya ligi misimu miwili iliyopita.


Msimu wa kwanza wa 2018/19, Simba Queens mchezo wa kwanza ilishinda mabao 7-0 na ule wa pili ilishinda kwa mabao 5-1.


Msimu wa 2019/20 ambapo Simba Queens iliweza kutwaa ubingwa ilishinda mabao 3-1 na ule wa pili ilishinda 5-1.


Mussa Mgosi, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wamejipanga kushinda mbele ya wapinzani wao kwa kuwa wana kikosi kipana chenye wachezaji wenye uzoefu.


Edna Lema Kocha Mkuu wa Yanga amesema anataka kuonyesha kwamba anauwezo wa kuifunga Simba ili kuweza kutwaa ubingwa.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic