December 4, 2020


UONGOZI wa Simba umesema kuwa nafasi walizopewa kwa ajili ya mchezo wa kesho wa marudio wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Plateau United hazitoshi jambo ambalo lilimfanya aseme kuwa wanampango wa kuwaruhusu mashabiki wa Simba wajitokeze kushangilia kwa wingi.


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wengi wamekuwa wakitafsiri vibaya jambo hilo kwa kuwa hawakuelewa maana yake aliposema kuwa wanahitaji mashabiki wa Simba wajitokeze kwa wingi kuishabikia timu hiyo.

Manara amesema:"Nafasi 30,000 hazitutoshi Simba kwa kuwa tuko wengi, ndio maana nilitaka waje Simba wengi kushangilia. Nafikiri kuna watu hawakunielewa makusudi au bahati mbaya.


“Ndio maana nimejitokeza na kusema tuwafundishe Yanga ustaarabu, kama ikitokea shabiki wetu ameingia tusilipe kisasi, lazima tuendeleze ule utamaduni wetu wa kujali na upendo kwa kila shabiki bila kubagua.

“Mashabiki wa Simba wamepigwa dhidi ya Azam, wamepigwa dhidi ya Mtibwa na wako ambao hawakusema. Sasa mashabiki wa Simba, wawafundishe hawa kwa ustaarabu,” amesema.

11 COMMENTS:

  1. Vyovyote itakavyokua Hadji.upo sahih binafs nakuunga mkono yann kuruhusu watu wasiojua nn maana y mpira?wanapiga wenzao wanafanya kila aina y fujo uzijuazo ni ushamba ulopitiliza kukataa wasije uwanjan naunga mkono hoja.bora uwe na wafuasi wachache wanaojieshim na kuthamin wenzao kuliko kua na wahuni wengi wanaoweza kuchafua brand na kusababisha tuonekane watu wa mpira ni wahuni wavuta bangi n.k mpka leo hi sijajua kwann tff imeshindwa kutoa adhabu kwa Tim y yanga ni ujinga kulea upuuzi kama huu unaofanywa na mashabiki wa yanga et kiss utaonekana unapenda Tim pinzan.narudia tena tunawakarubisha mashabiki wa yanga wanaojieshim wapenda mpira waje uwanjan kuangalia burudani wahuni wote wabaki t nyumban waangalie kwenye tv.

    ReplyDelete
  2. Kwasababu video ile ipo youtube, kila mwenye akili akisikiliza ataelewa, ndio maana TFF imekemea,na Simba ikatoa tamko juu ya kauli ile.
    Kitu cha kujifunza Kosa Moja alihalalishi Kosa jingine, Fifa wanakemea aina yoyote ya Ubaguzi

    ReplyDelete
  3. Haji uko sahihi kwanini tuzidi kuwa wanyonge kisa yanga no ,tuendelee kufanyiwa ujinga haitawezekana

    ReplyDelete
  4. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  5. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  6. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  7. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  8. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  9. Tafadhalini Sana tutumie lugha yenye ustarabu katika kutuma ujumbe... Lugha chafu haileti ladha katika mjadala Bali huleta karaha... watanzania huo ni mpira Tu usiwagawe..
    Mimi ni mmoja wa washabiki wa mpira wa Tanzania kutokea 1971...Naishi Kenya.Kwa sasa munapo elekea katika malumbano siko kuzuri..Unit of language must change..n be humble in Ur postings.

    ReplyDelete
  10. Manara kwa Ile kauli haikua sahihi wapo wenye mawazo finyu wapenda vurugu wanamuunga mkono kwamba aendelee na ubaguzi wake ktk soka sidhani kama no ushauri mzuri kwa Haji huo

    ReplyDelete
  11. Hakuna lolote baya ambalo ulizungumza Haji ... watu wanatafsiri vitu kwa mitazamo tofauti ... Wasamehe tu ..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic