December 1, 2020

 


KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amesema hana hofu ya kufukuzwa licha ya kuwa timu yake imeendelea kuwa na matokeo mabaya.

 Wolves iliifunga Arsenal mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Emirates, juzi na hivyo kuongeza presha kubwa kwa Arteta kwa kuwa ni kipigo cha tatu mfululizo kwenye uwanja wa nyumbani.

 

Arteta amesema:-“Siku ambayo niliamua kuwa kocha nilijua kuwa ipo siku nitafukuzwa na ninaondoka kwenye klabu.


“Sijui kama siku hiyo ni lini, miezi sita au mwaka au miaka tangu niliposaini mkataba, hivyo sijawahi kuwa na hofu ya kufukuzwa.

 

“Ninachojali kwa sasa ni kufanya wachezaji wangu wacheze vizuri, kufanya mazuri kwa timu ili kupata matokeo mazuri.

 

“Ninajua kwa taaluma hii ipo siku nitafukuzwa au nitaondoka mwenyewe, sijui lini itakuwa hivyo,” amesema kocha huyo.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic