December 1, 2020


 KAMPUNI ya michezo ya kubahatisha ya M-Bet imezindua kampeni mpya ijulikanayo kwa jina la ‘Ni Zamu Yako’  ambayo imekwenda sambamba na kukabidhi zawadi ya mshindi wa 94 wa Perfect 12, Samwel Humbe ambaye alizawadiwa Sh 145,351,400.

Meneja Masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi amesema kuwa kampeni hiyo inahamasisha mashabiki wa soka na watanzania wenye umri kuanzia miaka 18 kuendelea kubashiri na kuwa miongoni mwa washindi ambao watajishindia mamilioni ya fedha kupitia mchezo wa Perfect 12 na michezo mingine ya kubahatisha ya kampuni hiyo.

Mushi amesema kuwa mpaka sasa wametumia Sh4.2 billioni kuwazadia washindi mbalimbali kupitia mchezo wa Perfect 12 ambayo ulianza rasmi mwaka 2017.

“Humbe ni mshindi wa 94 tokea kuanza kwa mchezo huo wa kubahatisha wa Perfect 12  ambao umeweza kubadili maisha ya Watanzania wengi hapa nchini. Kampeni mpya inahamasisha zaidi mashabiki kuendelea ‘kubeti’ kupitia M-Bet ambayo kwa sasa imeweza kuwapa maendeleo mashabiki wa soka na kujiunga na nyumba ya mabingwa,” amesema Mushi.

Kwa upande wake, Humbe ambaye ni shabiki wa Yanga amesema kuwa atatumia fedha hizo kuanzisha  biashara mpya huku akiwasomesha watoto wake.

Amesema kuwa pia ataendeleza kazi yake ya ufundi seremala kwa kununua vifaa vya kisasa na kuifanya kazi yake iwe ya kisasa.

“Nimefurahi sana kushinda, sikuamini kupata ushindi huu ambao kwa ujumla, naipongeza kampuni ya M-Bet kwa kuwa wakweli na mshindi anapatikana kwa mujibu wa sheria,” amesema Humbe.

Mkuu wa kitengo cha michezo ya kubahatisha mkoa wa kodi wa Ilala, Shaaban Mwanga alimpongeza Humbe kwa ushindi na kampuni ya M-Bet kwa kutimiza wajibu wake ikiwa pamoja na kulipa kodi za Serikali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic