ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage amemtaka kocha mkuu wa timu hiyo, Sven Vandenbroeck kwenda na tahadhari ya juu kuwakabili Platinum FC ya Zimbabwe kwa kuwa ni wazuri kuliko Plateau United ya Nigeria.
Simba imefanikiwa kutinga katika hatua ya kwanza ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuwaondoa Plateau United ya Nigeria kwa jumla ya bao 1-0 na sasa wanatarajiwa kucheza ugenini na Platinum ya Zimbabwe Desemba 23, mwaka huu.
Rage amesema kuwa, Simba chini ya Sven raia wa Ubelgiji wanatakiwa kujiimarisha zaidi kadiri siku zinavyokweda kwa kuwa wapinzani wao Platinum ni wazuri ukilinganisha na Wanaigeria.
“Simba inatakiwa ijipange vizuri katika hatua waliyofi kia kwani timu wanayokwenda kukutana nayo ni nzuri zaidi ya Wanaigeria waliopita hivyo hawatakiwi kuibeza hata kidogo, wanatakiwa wajipange kuhakikisha wanafanya vizuri.
“Kikubwa ninachokiona mimi waende wapambane wapate bao moja kisha walinde goli lao naona itakuwa na manufaa zaidi.
“Michuano hii jinsi ilivyo, kadiri unavyopiga hatua ndio mashindano yanavyokuwa magumu zaidi kwa kuwa unakutana na timu bora, hivyo wanahitaji kujipanga,” amesema Rage.
Nasaha hii isiwe magazetini tu lakini nashauri kuwa Mzee Rage akutane na kocha uso kwa uso na kumpa Nasaha hizo na tu naitakia Simba kila la kheri
ReplyDeleteNi kweli kabisa. Ila huyu kocha KWA mimi naona timu ni kubwa kushinda YEYE.
DeleteMSICHUKULIE POA, NYUMBA CHOO, ACHA KUISHI KWA MAZOEA KATIKA SOKA, MPIRA NI MBINU TU. UNADHANI WAKINA GUARDIOLA WANAOLIA WAO WAJINGA? NA KWANINI WANAKUBALI MATOKEO? KATIKA LIGI SIMBA INAHUJUMIWA NA WAAMUZI TU NA SIO KINGINE
DeleteHapa ilipo ndiyo sahihi masuala ya kuzungumzia chumbani si mema sana, kwa sasa tunahitaji viongozi wa aina hii sio wa kukosoa tu.
ReplyDeleteNi ukweli usiopingika kwamba Platinum Fc ya Zimbabwe ni Timu nzuri na bila Simba kujipanga kwenda hatua nyingine itakuwa ndoto ya mchana.
Tunakushukuru Mzee Rage kwa kutoa ushauri wa maana kwa wakati sahihi. Ubarikiwe sana.
SOKA LA AFRIKA MTU KWAO, WAKIWEZA KUSHINDA HUJUMA NJE YA UWANJA, WAKIINGIA UWANJA NI MPIRA SPANA TU WATATOBOA. KAMA ILIVYOKUWA NIGERIA, HII NI AFRIKA
Delete