IMEBAINIKA kuwa kiungo mshambuliaji hatari wa Klabu ya Simba, Luis Miquissone amegoma kuondoka ndani ya timu hiyo licha ya matajiri wa Kiarabu kutoka nchini Misri, Klabu ya Pyramids kuonyesha nia ya kuhitaji huduma yake.
Pyramid inaripotiwa kuwa tayari kuvunja mkataba wa Luis na Simba kwa kuweka mezani dau linalokadiriwa kufikia shilingi Bilioni 1.5 za Kitanzania.
Akizungumzia ofa hiyo mmoja wa viongozi wa juu wa klabu hiyo aliyeomba hifadhi ya jina lake amesema Luis alikaa kikao na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohammed Dewji 'MO' ili kujadili dili hilo, lakini akamjibu bosi huyo kuwa ana furaha kuendelea kuitumikia Simba na wala hana mpango wa kuondoka ndani ya timu hiyo kwa sasa.
"Suala la Luis kuhitajika na Pyramid ni kweli lipo na tayari walishaleta ofa ambayo ilijadiliwa kwa kirefu na Mwenyekiti wa Bodi ambapo, Luis alipewa taarifa ya uwepo wa dili hilo.
"Lakini Luis mwenyewe alimwambia MO kwamba bado ana furaha kuendelea kuichezea Simba kwa misimu mingi zaidi na kwa sasa hana mpango wa kuondoka Simba,".
Huyo ndie muungwana anaejuwa fadhila na akaona utu na uaminifu ni bora kuliko pesa
ReplyDeleteAnaipenda simba na ni muungwana sana
ReplyDeleteMuache asubiri wamchoke,atakuja likumbuka hilo dili,hawajui Simba na Yanga huyo
ReplyDeleteKweli atajuta sana, hizi timu zetu ni kama Bublish tu, ukiish autamu watu wanatema mbali huko.
DeleteFigisu ti hakuna cha kukataa wala nn na nyie mmegeuka utopolo kuwafungia milango wachezaji bumbavu
ReplyDeleteBiashara nzuri sana hii kwenye soka basi tu wabongo hatujitambui
ReplyDeleteKuna kuondoka anafka pyramid yanamkuta ya kichuya
ReplyDeleteBora akae tu huenda thaman yke ikapanda zaid
Simba hawa wakatae daunla B1.5 thubutu huyo konde hakifikisha hata 200m acheni kuandika porojo na upuuzi
ReplyDeleteHakuna hapa Tanzania club itakayokataa kumuuza mchezaji kwa ofa ya bilioni 1 na nusu, Hawa jamaa wanapika Sana Habar
ReplyDeleteSimba kama wataacha b1.5 basi watakua hawajui maana halisi ya biashara ktk mpira
ReplyDeleteMi simba damu kama kweli IPO iyo of a ya b1.5ni kuchukua tu binge LA biashara hyo
ReplyDeleteThamani ya miqson ni kubwa mno bilioni1.5 ni hela kdogo sana,,,kwanza simba wenyewe wamelipa mil700 kuvunja mkataba mamelod sundown bado hela yake ya usjaili kamq zaid ya mil300 alizochukua yy kama mchezaji ,,,,iyo itakua biashara bubu simba wametumia zaidi ya bilion moja kumsajili aje amuuze kwa bil1.5??hamnaga biashara ya kiboya kama iyo,,,simba akifanikiwa kuingia makundi na miqson akikiwaya sana simba watakuja kumuuza kwa zaidi ya bilion4 za kitanzania
ReplyDelete