December 4, 2020


 MCHEZAJI wa kimataifa wa Tanzania, Adi Yussuf anayekipiga katika Klabu ya Wrexham Association FC ya Wales kwa mkopo akitokea Boreham Wood FC ya England, amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi 
Novemba.

 

Adi ametwaa tuzo hiyo baada ya kuweka kambani mabao manne katika michezo nane aliyocheza hadi sasa, kwenye mashindano ya National League ambayo ni sawa na Ligi Daraja la Tano katika mfumo wa soka la Kiingereza ambayo ilianzishwa mwaka 1864.

 

Nyota huyo aliwahi kuitwa mara kadhaa kwenye kikosi cha Taifa Stars wakati wa kocha Emmanuel Amunike, akiwa miongoni mwa wachezaji ambao walikwenda Misri kushiriki Afcon, mwaka jana na kupata nafasi ya kucheza mechi moja.


Ni miongoni mwa washambuliaji wazawa amabao wanapeperusha bendera ya Tanzania nje ya nchi jambo linaloifanya Tanzania kuzidi kupasua anga taratibu kitaifa na kimataifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic