December 22, 2020


 UONGOZI wa Dodoma Jiji umesema kuwa utapambana kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa kesho, Desemba 23.

Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Jamhuri, unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa timu zote zinahitaji pointi tatu muhimu.

Akizungumza na Saleh Jembe, katibu wa Klabu ya Dodoma Jiji, Fortunatus amesema kuwa tayari kikosi kimeweka kambi Morogoro na wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo huo.

"Tupo Morogoro kwa sasa na kikosi kinaendelea na mazoezi ili kuweza kupata matokeo kwenye mchezo wetu huo.


"Kila mchezaji anajua kwamba tunahitaji ushindi na ili tushinde ni lazima tucheze kwa juhudi ili kufikia malengo ambayo tumejiwekea," amesema.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic